TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri (MAB) na  Watendaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) pamoja na mameneja wa Kampasi wamepewa Mafunzo maalumu ya Utawala bora

May 3, 2021
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri (MAB) na  Watendaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) pamoja na mameneja wa Kampasi wamepewa Mafunzo maalumu ya Utawala bora yaliyotolewa na Taasisi ya wakurugenzi (Institute of Directors.) Katika Ukumbi wa mikutano wa Bunge jijini Dar es salaam kwa mda wa siku mbili kuanzia leo tarehe 03/05/2021 hadi 04/05/2021

Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha utawala bora wa  maendeleo ya TIA  na kujenga maslahi bora kwa serikali, watanzania kwa kuzingatia ushirikiano na kutimiza wajibu kwa Bodi ya Ushauri ya Taasisi na Utawala.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wakuu  wa kampasi wa Taasisi ya TIA kutoka mikoa ya Mbeya, Mwanza, Kigoma, Singida na Mtwara pamoja na Dar es salaam.

Picha za  Wajumbe wa Bodi ya  Ushauri (MAB), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, DRAC, DRFPA, Mameneja wa Kampasi za TIA pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali za TIA