Tangazo kwa wahitimu wa kidato cha nne 2016 walioomba kujiunga na chuo – March Intake 2017

Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) inapenda kuwataarifu wanafunzi waliomaliza kidato cha nne 2016 ambao waliomba kujiunga na Taasisi (March Intake 2017) katika Kampasi za Dar es Salaam, Mbeya, Singida, Mtwara, Mwanza na Kigoma kwamba, kufuatia maelekezo ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), hawataweza kujiunga na chuo katika kipindi hicho; badala yake watajiunga na chuo kwenye Mwaka wa Masomo 2017/2018 utakaoanza Mwezi Augosti 2017.

Aidha waombaji ambao awali waliomba kwa kujaza fomu na kulipia kwa njia ya M-Pesa, kisha kurejesha fomu kwenye Kampasi zetu; hawatahitaji kutuma tena maombi/kulipia gharama za maombi (Application Fee).

Taasisi inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia:

Simu:

Dar es Salaam: +255 22 2850717

Mbeya: +255 25 2502276; 0754297971/0621135622

Singida: +255 26 2502125; 0754486044/0763126876

Mtwara: +255 23 2333948; 0754619019/0754422381

Mwanza: +255 28 2570475; 0754443930/0767418241

Kigoma: +255 28 2803529; 0755397449/0763517322

 

Barua-pepe: tia@tia.ac.tz

Tovuti: www.tia.ac.tz

 

IMETOLEWA NA IDARA YA UDAHILI,

TAASISI YA UHASIBU TANZANIA.

03 APRILI 2017